1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Xi Jinping wa China akutana na viongozi wa Ulaya

Zainab Aziz
7 Desemba 2023

Viongozi wa Umoja wa Ulaya na wa China wamekutana leo mjini Beijing baada ya miezi kadhaa ya mivutano ya kibiashara baina yao.

https://p.dw.com/p/4ZsLa
China Peking 2023 | vor 24. EU-China-Gipfel | Xi Jinping mit  Ursula von der Leyen & Charles Michel
Rais Xi Jinping, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen na Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel.Picha: Dario Pignatelli/European Council Press Service/AFP

Rais wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, akiwa na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel na mkuu wa sera za nje wa Umoja  huo Josep Borrell, wamesema zipo tofauti ambazo ni lazima zitatuliwe kati ya Umoja wa Ulaya na China, mshirika mkubwa wa kiuchumi wa Umoja wa Ulaya. China na Umoja wa Ulaya zimeongeza ushirikiano wa kidiplomasia mnamo mwaka huu, zikitaka kuharakisha kurekebisha uhusiano wao. Maafisa kadhaa wa Umoja wa Ulaya wameitembelea Beijing mara kwa mara ili kuanzisha upya mazungumzo ya ngazi ya juu.