1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji wa Hamas waelezwa kuishambulia Isreal

Zainab Aziz
7 Desemba 2023

Jeshi la Israel limesema wapiganaji wa kundi la Hamas wamerusha makombora kadhaa kuishambulia Israel kutokea kwenye eneo lililotengwa kwa ajIli ya usalama wa raia kusini mwa Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ZtLg
Gazatreifen | Zerstörung in Rafah
Watu wanaangalia sehemu iliyoshambuliwa na makombora ya IsraelPicha: MOHAMMED ABED/AFP/Getty Images

Wapiganaji hao wameripotiwa kurusha makombora kutoka kwenye eneo lililo karibu na vituo vya Umoja wa Mataifa na kusababisha raia wayakimbie mahema yao katika eneo la al-Mawasi kwenye Bahari ya Mediterania karibu na mpaka wa Misri. Jeshi la Israel limesema Hamas walirusha makombora 12 kuushambulia mji wa Beersheba wa kusini mwa Israel na kombora moja liliangukia ndani ya Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel mara kwa mara limewalaumu Hamas kwa kuwatumia raia wa Gaza kama ngao, madai ambayo kundi la Hamas limekanusha.