1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FC Cologne waondoka kwa muda kutoka eneo la kushushwa daraja

2 Desemba 2023

Davie Selke alifunga goli la ushindi usiku wa kuamkia leo klabu yake ya FC Cologne ilipopata ushindi wa 1-0 dhidi ya Darmstadt.

https://p.dw.com/p/4ZhfS
FC Cologne waondoka kwa muda kutoka eneo la kushushwa daraja
FC Cologne waondoka kwa muda kutoka eneo la kushushwa darajaPicha: Lars Baron/Getty Images

Davie Selke alifunga goli hilo katika dakika ya sitini ya mechi kupitia kona na kuipelekea timu yake kutoka kwa muda kutoka kwenye eneo la kushushwa daraja.

Hii leo ndio idadi kubwa ya mechi za Bundesliga zitakapochezwa ambapo mabingwa Bayern Munich watakuwa wanachuana na Union Berlin kisha mechi itakayokuwa inasubiriwa na wengi itakuwa siku ya Jumapili kati ya vinara wa sasa Bayer Leverkusen watakapowaalika Borussia Dortmund.